Mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo, ametoa siku 30 kwa wafugaji waliovamia maeneo ya wakulima mkoani humo kuondoa mifugo yao mara moja.

Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza, Wilaya ya Bagamoyo, amesema kuwa hataki kuona mifugo mipya ikiingizwa mkoani humo kwani inatosha na ina sababisha migogoro.

Aidha, Ndikilo amewaasa viongozi na watendaji mbalimbali kuanzia ngazi ya kijiji, kata, wilaya na wakurugenzi, kuwa wakali na kusimamia kidete kukomesha uingiaji holela wa mifugo katika maeneo yao.

Hata hivyo, Ndikilo amewataka wafugaji kuacha mara moja tabia ya kuwanyanyasa wakulima na kusisitiza kuwa kila mwananchi anapaswa kutii sheria za nchi.

Serikali kulipa madeni yote ya Maliasili
Gutteres atamani 2017 uwe wa amani duniani