Mume wa muigizaji wa Filamu za Kibongo Irene Uwoya ambaye ni mchezaji wa timu ya mpira Rwanda Hamad Ndikumana amefunguka na kusema amechoshwa na skendo za mke wake hivyo yupo tayari kumpa talaka mwadada huyo ili aendele kuishi maisha anayoyataka yeye.

Uamuzi huo umefanyika baada ya Irene Uwoya kukutwa na skendo nyingi ambazo zilimfedhehesha Ndikumana na kujikuta akiruhusu Uwoya kuolewa kwingine na kuishi maisha anayotaka.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ndikumana ameandika ujumbe na kukubali kumpa talaka mwadada Irene Uwoya.

“Ulilia muda kwamba unataka talaka ili uolewe, sina kipingamizi tafuta kila utakacho ulete nitakusainia, usisubiri nife ili uolewe maana naweza kuishi zaidi ya unavyofikiria, Mungu akusimamie”, aliandika Ndikumana.

Pia Ndikumana amesema kitendo cha Irene kumnyima kuzungumza na mwanae tangu watengane, ni kitendo kinachomuumiza sana, lakini yote anamuachia Mungu.

“Ungekuwa na roho ya kibinadamu ungekuwa unataka hata niwasiliane na mtoto, ila miaka miwili hujawahi chukua simu unipigie umpe mtoto niongee naye, hata picha tu hutaki nitumia ila naelewa kwa nini unafanya hivyo, na baada ya yote haya hutotaka nimuone tena, lakini ni sawa Mungu yupo na ipo siku”, aliendelea kuandika Ndikumana.

Irene na Ndikumana walifunga ndoa mwaka 2009 na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume, lakini ndoa yao haikudumu muda mrefu na kutengana, hivyo sasa Ndikumana ameonyesha kuridhia kutoa talaka kwa msanii huyo wa bongo movie.

Kinana ampa tano Museven, asema hakuna Rais duniani kama yeye
Sababu ya kuvunjika ndoa ya Nuh Mziwanda yatajwa