Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu jana usiku amevalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa kituo cha Radio cha EFM Francis maarufu kama Majizo.

Tukio hilo lilitokea jana usiku kwenye sherehe ya watoto wao, ambapo Lulu alifanyiwa ”Suprise” ya kuvalishwa pete.

Kimepita kitambo kirefu tangu kuachiliwa kwa Lulu aliyekuwa anatumikia kifungo ndani na nje mara baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na mauaji ya muigizaji mwenzake Steven Kanumba.

Tangu kuachiliwa kwake Lulu amekuwa kimya hasa mitandaoni, kimya hiko kilivunjwa baada ya tetesi zilizoanza kusambaa mitandaoni zikidai kuwa hivi karibuni Lulu na Majizo wanatarajia kufunja ndoa.

Yai hilo lilipasuliwa kwa mara ya kwanza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ambaye kwenye ukurasa wake wa Instagram alijitangaza kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya ndoa inayotarajiwa kufungwa na wawili hao.

 

Lugola ashusha rungu polisi, ''Marufuku kushindwa kutoa dhamana''
Video: CCM yaingia hofu 2020, Vigogo watumbuliwa wizara ya elimu

Comments

comments