Wakati wa Salum ‘Abo’ Telela kuondoka Young Africans umefika na taarifa zinaeleza, benchi la ufundi limeridhia.
Mkataba wa Young Africans na Telela umeisha, lakini inaonekana hakuna mpango wa kumuongeza usajili.
Kawaida ya Young Africans kama inamhitaji mchezaji basi hata kabla wake kwisha, huwa inamalizana naye mara moja.
Safari hii utaona, hadi mkataba wa Telela unamalizika kabisa.
Young Africans wamekuwa kimya ingawa imearifiwa, tayari Telela ameelezwa kwamba yuko huru.
Ratiba Ya Ligi Ya England Msimu Wa 2016-17 Yaanikwa Hadharani
Picha: Poulsen Na Shime Waanza Program Ya Kuwavaa Shelisheli