Ndoto ya Mabingwa wa soka msimu huu kutoka nchini Tanzania Klabu ya Simba ya kusafiri kwenda Uingereza kucheza na Klabu ya Everton imeota mbawa mara baada ya kuchezea kipigo cha goli 2- 0 kutoka kwa mabingwa wa soka nchini Kenya Gor Mahia.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali na wa kusisimua, Gor Mahia walikuwa wa kwanza kupata bao mara baada ya kupachika goli kipindi cha kwanza.

Aidha, katika mchezo huo ambao ulionekana kwa Simba kuzidiwa katika kila Idara umemalizika kwa Gor Mahia kuondoka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya mabingwa wa ligi Kuu Tanzania Bara, Klabu ya Simba.

Hata hivyo, Simba imeshika nafasi ya mshindi wa pili mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ya SportPesa yaliyofanyika nchini Kenya.

 

Lil Wayne, Birdman wakunja makucha, wajipanga upya
Video: Terrence ‘ampasua’ aliyempiga Manny Pacquiao

Comments

comments