Rais wa klabu bingwa nchini Ufaransa PSG, Nasser Al-Khelaifi amefungua milango kwa mshambuliaji wa Colombia na klabu ya Real Madrid, James Rodriguez kuwa na urahisi wa kucheza soka lake nchini England kuanzia msimu ujao wa ligi.

Al-Khelaifi amedhihirisha suala hilo baada ya kukanusha taarifa za klabu ya PSG kuwa na mipango ya kumsajili mshambuliaji huyo ambaye aliibuka kidedea katika tuzo ya ufungaji bora wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.

Al-Khelaifi, amesema taarifa zilizotolewa na Real Madrid kuhusu mazungumzo yanayoendelea kati yao na PSG, hazina ukweli na alishangazwa kuzisikia kutokana na James kutokua katika mipango ya kujiunga na klabu hiyo ya jijini Paris.

“Hakuna ukweli wowote kuhusu jambo hilo, kilichozungumza na Real Madrid sio sahihi, hatukuwahi kuzungumza nao kuhusu James hata siku moja,” Alisema Al-Khelaifi

PSG tayari wameshamsajili Hatem Ben Arfa, kama mchezaji huru akitokea Nice, na huenda jambo hilo ndio limempa kiburi Al-Khelaifi kutangaza maamuzi ya kutomfikiria James.

Kutokana na kauli hiyo ya Al-Khelaifi, kuna uwezekano wa meneja mpya wa Man Utd, Jose Mourinho kukamilisha mipango ya usajili wa James Rodrigues kwa urahisi kutokana kuwa na matamanio ya kumjumuisha kikosini mwake kuanzia msimu ujao.

Rodrigues, anahusishwa na mpango wa kuondoka Estadio Santiago Bernabeu katika kipindi hiki, kutokana na kushindwa kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane tangu alipokabidhiwa kikosi msimu uliopita mara baada ya kuondoka kwa Rafa Benitez.

Everton FC Yamuwinda Thomas Henry Alex "Hal" (Robson-Kanu)
Cristiano Ronaldo: Siamini Kama Lionel Messi Amestaafu