Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo Mei 7, 2021 amesisitiza kuhusu wabunge 19 waliofukuzwa uanachama Chadema, huku akitaka kupatiwa vielelezo kuhusu kufukuzwa kwao na kwamba huo ni msimamo wa kiti.

Wabunge hao 19 akiwemo Halima Mdee walifukuzwa CHADEMA Novemba mwaka 2020 baada ya kuapishwa kuwa wabunge bila ridhaa ya chama hicho lakini wameendelea kuwa wabunge jambo ambalo kwa nyakati tofauti CHADEMA wamelipinga huku Ndugai akidai hana vielelezo.

“Maamuzi ninayotoa hapa, ni maamuzi ambayo yatatumika nami na hata watakaofuata baada yangu… Kwa vyama vyovyote vyenye kufukuza wabunge…. wanapaswa wanapomwandikia barua spika… lazima barua hiyo iambatane na katiba yao, iambatane na muhtasari au mihtasari ya vikao vilivyohusika kuwafukuza wabunge hao,” amesema Spika Ndugai. 

Aidha, Ndugai amesema kuwa angalizo hilo haliwalengi wabunge wa upande mmoja tu bali kwa chama chochote cha siasa  ambacho kitakuwa na nia ya kuwatimua wabunge.

Hata hivyo Ndugai amerejea kauli yake kuwa hayupo kwa ajili ya kufukuza wabunge bali kuwalinda.Bunge lakosa maswali kwa Waziri Mkuu

VIDEO: Mkutano wa Rais Samia Suluhu Hassan na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam
Waziri Mulamula akutana na mabalozi wanne, kupokea hati za utambulisho