Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Job Ndugai amemtangaza mbunge wa Bunda (Chadema), Easter Bulaya kuwa ndiye anayekalia kiti cha Mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni.

Katika mkutano wa 18 wa Bunge kikao cha kwanza ulioanza leo Januari 28, 2020, Spika Ndugai alimtangaza Mbunge Bulaya kuwa amepokea jina hilo kutoka kwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani, Freeman Mbowe.

Bulaya amechukua nafasi ya aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ambaye alivuliwa ubunge mwaka jana.

Kabla ya uteuzi huo, aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo ni Joseph Selasini mbunge wa Rombo (Chadema) ambaye alijiuzuru nafasi hiyo wiki iliyopita.

Aidha, mbali na kumtangaza Bulaya, Spika Ndugai alimpongeza Mbowe kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine kuwa mwenyekiti wa Chama Chadema.

Mama Sitta aangusha kilio bungeni akipokea joho la marehemu mumewe
Bunge laanzisha kwaya, imetumbuiza leo

Comments

comments