Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameunda kamati mbili zitakazoshughulikia sekta ya Uvuvi na Gesi ili kuweza kujua ni kwa nini hazichangii pato la taifa.

Ndugai ameunda kamati hizo baada ya zingine mbili za kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi. umiliki na usimamizi wa madini ya Tanzanite na almasi kuwasilisha taarifa kwa Rais Dkt, John Magufuli na kusababisha baadhi ya mawaziri kujiuzulu.

Akitangaza kamati hizo bungeni mjini Dodoma, Ndugai amemrejesha Dotto Biteko aliyekuwa mwenyekiti wa kamati iliyochunguza madini ya Tanzanite kuwa mwenyekiti wa kamati itakayochunguza sekta ya gesi.

Amesema kuwa hali ya kusuasua katika sekta hizo unahitaji kufanyiwa utafiti ili kuweza kuona ni namna gani zitaweza kuchangia pato la taifa.

Hata hivyo. Ndugai amemuagiza Katibu wa Bunge kuwawezesha wabunge hao ili waanze kazi mara moja na kamati hizo zimetakiwa kufanyakazi ndani ya siku 30 tangu zilipokabidhiwa majukumu.

 

Video: Rais Mugabe king'ang'anizi aisee, Bombardier pasua kichwa Canada
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 18, 2017