Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewataka watanzania kuwa na uvumilivu wa masuala ya kidini ili nchi iendelee kuwa na amani, utulivu na maendeleo.

Ameyasema hayo Wilayani Kondoa mkoani Dodoma, alipokuwa akizungumza wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an yaliyowashirikisha zaidi ya watoto na vijana 40 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Amesema kuwa umoja na mshikamano uliopo hapa nchini ni matokeo ya viongozi wa dini mbalimbali hapa nchini kuendelea kuhubiri amani na utulivu na kuitaka jamii na viongozi hao kuiendeleza kazi hiyo.

“Waziri wa Mambo ya Ndani anafanya kazi ya kuangalia shughulia za kidini ndani ya  nchi yetu zinandelea kwa amani kati ya dhehebu na dhehebu, endeleeni kuhubiri amani kila siku. Kazi iliyoifanywa na nyie Masheikh ni kubwa mno kwani kama amani mmeihubiri na tayari watanzania wameshaishika.  Watanzania wanauvumilivu wa kipekee sasa inabidi kuhubiri uvumilivu wa kidini,”amesema Ndugai

 

Beki wa kituruki akaribia kaskazini mwa London
Magazeti ya Tanzania leo Juni 11, 2018