Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa linamshikilia mwanamke mmoja mkazi wa Msata, Pwani, kwa tuhuma za kumuiba mtoto wa wiki 1 wa nduguye, Samia Ruhusa (35).

Kamanda wa polisi mkoani humo, Justine Masejo, Siku ya tukio, Juni 11, mtuhumiwa alimpigia simu mama wa mtoto na kumwambia aende kutoa hela aliyomtumia usiku huo ili kumsaidia.

Mama wa mtoto alipoenda kutoa hela, mtuhumiwa alimchukua mtoto na kuchoma moto godoro ili ionekane kuwa mtoto ameteketea kwa moto. Baada ya tukio, majirani na mama wa mtoto walitoa taarifa Polisi.

Kamanda Masejo amesema kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kumkamata mama huyo na alipohojiwa alikiri kufanya tukio hilo la kumuiba mtoto na kutoroka naye.

Mwanamke huyo amesema kuwa sababu ya kumuiba mtoto huyo ni kwa kuwa ametafuta mtoto kwa muda mrefu bila mafanikio.

RPC Arusha ahamishwa kituo cha kazi
Young Africans watuma ofa Coastal Union