Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), kupitia Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi na haki za Kisheria Lina Msanga amesema kuwa idadi ya wanandoa wanaopeana talaka imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka na kutaja baadhi ya sababu zinazochangia hali hiyo.

Msanga amesema takwimu za talaka zilizopo Rita ni zile zilizopokelewa kutoka mahakamani ingawa huenda kukawa na talaka nyingi zaidi ambazo hazijawafikia.

”Mwaka 2016 januari hadi Disemba talaka ambazo tumezipokea na kuzisajili ni 110 na mwaka 2017 zimeongezeka hadi kufikia 127” amesema Msanga.

Moja ya sababu ambayo Msanga ameitaja kama chanzo cha ongezeko la talaka amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakioana bila kuchunguzana hivyo hutofautiana ndani ya muda mfupi.

”Watu hawachunguzani kufahamu mila na desturi za kabila anakotaka kwenda,” mfano unajua kuna makabila wanawake hawaruhusiwi kuongea na makabila mengine na makabila mengine wanaruhusiwa kuongea” amesema Msanga.

Ametaja sababu nyingine kuwa kuna watu wanakutana kwenye mitandao ya kijamii na kuanza mahusiano humo wakiamini wanaweza kuishi kama mume na mke bila kuwashirikisha wazazi ama ndugu wa karibu.

Sababu nyingine ni magubu ya dada za mume na ndugu za upande wa mke au mume kuhamia au kwenda mara kwa mara nyumbani kwa wanandoa na kusababisha upande mmoja kukereka.
Sababu nyingine ametaja kuwa wanawake kuachiwa majukumu na wanaume, amesema kuwa

Msanga ameongezea kuwa ”mwanzoni mwa mahusiano mwanaume huonyesha kuwa mwenye uwezo wa kutunza familia mnapoingia kwenye ndoa mwanaume husitisha huduma na kumuachia mwanamke majuku yote ya familia”

Subalkheri kuwatia mahakamani Aslay na Nandy
Lowassa atoa neno zito kwa Serikali

Comments

comments