Mwanyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Hashim Rungwe ameliomba jeshi la polisi kusaidia upatikanaji wa Mpwa wake Saida Hilal (40) na mumewe Abdallah Kutiku ambao hawajaonekana tangu Machi 26, 2018 majira ya asubuhi.
 
Hashim Rungwe amesema kuwa Saida Hilal aliaga wenzake ofisini na kwenda kituo cha polisi kufuatilia suala la mume wake Abdallah Kutiku ambaye alichukuliwa na polisi.
 
“Huyu binti alikuwa anafuatilia habari za mumewe polisi kwa kuwa mumewe alikuwa amekamatwa na polisi hivyo naye hapatikani kwa hiyo wote wawili hawaonekani kwani tulipofika kituo cha polisi walisema hawa watu hatuwafahamu na wala hawajafika pale, tangu hapo Bi. Saida Hilal hapatikani kwenye simu zake na tumefanya jitihada kumtafuta kwenye vituo vya polisi na mahospitali kama Muhimbili, Mwananyamala na sehemu zingine za usalama bila mafanikio,”amesema Rungwe
 
Hata hivyo, Rungwe amesema kuwa sehemu zote ambazo alikuwa anapenda kutembelea wamepita na hawajafanikiwa kumuona hivyo anaomba vyombo vya dola kusaidia kuwatafuta na kama wanashikiliwa kwa mujibu wa sheria anaomba wajulishwe ili waondokane na hofu kwani binti huyo ana watoto watano na anafanya kazi tume ya taifa ya uchaguzi.
 
  • Msemaji wa Serikali atolea tamko waraka wa baraza la KKKT
  • Video: Shaka afunguka kuhusu kung’olewa kwa Joketi UVCCM
  • Serikali kugharamia mazishi kijana aliyefariki Mbeya

Jacqueline amwandikia ujumbe mzito mume wake, Reginald Mengi
Video: Shaka afunguka kuhusu kung'olewa kwa Joketi UVCCM