Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Faustine Ndugulile amepiga marufuku uuzwaji wa vifaa vya kupimia virusi vya ukimwi kwa watu binafsi akidai kuwa sheria ya nchi hairuhusu mtu kujipima mwenyewe ugonjwa huo.

Agizo hilo ametoa leo Agosti 2o, 2018 katika hafla ya kukabidhiwa cheti cha ubora cha kimataifa cha ISO Kwa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Ndugulile amesema kwa mujibu wa sheria iliyopo inaruhusu mtu kupimwa virusi vya ukimwi na mtaalamu kutoka kituo cha afya na si vinginevyo

”Hivi sasa bado tupo kwenye hatua ya kubadilisha sheria hii ili tuweze kuruhusu watu kujipima wenyewe lakini itakuwa mara baada ya majaribio yatakayofanywa katika maeneo fulani na kuonyesha matokeo chanya” amesema Ndugulile.

Aidha ameziagiza Taasisi kuhakikisha wanadhibiti uuzaji holela wa vifaa vya kujipima ukimwi katika maduka ya dawa nchini kote.

Museveni asema Bobi Wine hakujeruhiwa, amnukuu Trump
Makala: Kwa mwendo huu, Rich Mavoko ‘kazi anayo’ (Video)