Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile amesema majibu ya vipimo vya magonjwa ya Typhoid na Urinary Track Infection (U.T.I) mara nyingine huwa si ya kweli kwasababu yanachukua muda mfupi wa masaa hadi 2 kutolewa.

Amesema kuwa kitaalamu vipimo hivyo huchukua masaa 48 hadi 72 kutoa majibu lakini kwenye maabara nyingi hapa nchini vipimo vya magonjwa hayo huchukua chini ya masaa mawili na kuongezea kuwa 70% ya homa ni virusi ambavyo tunavipata baada ya saa tatu au saba vinapotea.

“Ukitaka kupima typhoid kitaalamu unatakiwa kuchukuliwa damu iende maabara ikapandikizwe, ije iangaliwe vimelea vilivyoota…majibu haya yanachukua saa 72, si muda mfupi kama tunavyoshuhudia kwenye maabara nyingi,” amesema na kuongeza.

Aidha, amesema kwa sasa malaria imepungua sana hapa nchini na si kweli kwamba kila anayeumwa mwili ana malaria

“Watu wengi wanakwenda maabara wanasema wanasikia homa au viungo vinauma au mwili uko ovyo, wanaambiwa una malaria…Hii si kweli kwa sababu malaria ni kidogo sana na kwa sasa hivi wastani wa taifa ni asilimia 14 pekee ya watu wanaougua malaria,”

“Juzi kuna msichana alipewa dawa nne, hii si sahihi, mtu anachokifanya anapiga risasi zote kwa kutaka kuua sisimizi, lakini kama una homa unakwenda kwa daktari anakuandikia dawa ya malaria, dawa ya kupunguza homa, Antibiotic na dawa ya kuchua, jua huyo siyo daktari, huyo ni mganga wa kienyeji,” amesema Naibu Waziri.

Marais wa Korea Kaskazini na Kusini wakutana
Watakaoshiriki fainali za U17 wafahamika rasmi

Comments

comments