Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wananchi kutoa taarifa kwa hospitali yeyote inayotoza fedha kwa ajili ya matibabu ya wajawazito wanaokwenda kupatiwa matibabu kwa kuwa huduma hizo zinatolewa bure.

Ndugulile amefafanua kwa kutumia muongozo uliopitiwa mwaka 2009-2010 ambao umeweka bayana kuwa mara tu  mwanamke anapokuwa mjamzito huduma zote kuanzia kliniki ya wajawazito, au akiigua maradhi yeyote pamoja na huduma ya kujifungua, kumuona daktari, kupatiwa vipimo, kupatiwa dawa na kufanyiwa upasuaji pale itapo hitajika, hospitali iwajibike kutoa huduma hizo bure.

Tamko hilo limetolewa leo katika mkutano wa 10 kikao cha tano cha Bunge kinachoendelea jijini Dodoma.

Hayo yameelezwa alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa viti maalumu, Hawa Mchafu Chakoma alipohoji serikali kuhusu matibabu ya bure kwa wamama wajawazito.

Mama wajawazito ni moja ya makundi maalum wanapaswa kupata huduma za matibabu bure kama ilivyoainishwa katika muongozo wa uchangiaji wa huduma za afya mwaka 1997. Wakina mama wajawazito ni haki yao kupewa huduma zote bila ya malipo na sio zile tu zinazohusu ujauzito“, amesema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Ndugulile amesema wizara ya afya imeandaa bajeti ya kununua vifaa wanavyotakiwa kutumia wanawake wajawazito ili kuwaondolea adha wafika hospitalini.

 

Mgombea udiwani aliyepotea apatikana akiwa hajitambui
Kibarua cha meneja TRA chaota nyasi

Comments

comments