Mkali wa RnB, Ne-Yo amefunga ndoa Jumamosi, Februari 20 mbele ya familia yake na marafiki wachache huko Los Verdes, California nchini Marekani.

Ne-Yo amemuoa mchumba wake mwanamitindo, Crystal Renay  ambaye alisimama kula kiapo cha kuwa mke halali wa mwimbaji huyo akiwa na ujauzito wa miezi 9.

Ne-Yo ambaye ana watoto wawili aliozaa na mchumba wake wa zamani, Monyetta Shaw amesema kuwa aliamua kufunga ndoa na Renay baada ya kugundua kuwa ana kitu maalum na cha kipekee ambacho wanawake wengi hawana.

“Tunatamani kuanza maisha yetu pamoja. Tunasubiri kwa hamu kuwa marafiki wakuu katika uhusiano wetu,” Ne-Yo aliliambia PEOPLE.

Meya wa Kinondoni avutana na makonda
Nape atangaza Neema hii kwa waandishi wa habari