Mwanamuziki nyota kutoka nchini Marekani, Shaffer Chimere Smith maarufu Neyo hatimaye amevunja ukimya kufuatia mkewe Crystal Smith kuvujisha taarifa za familia mtandaoni, akidai kuwa ndoa ya wawili hao imevunjika kufuatia kukithiri kwa vitendo vya usaliti, vinavyofanywa na mwimbaji huyo kwa karibu kipindi chote cha ndoa yao.

Kitendo cha kuenea kwa kasi kwa taarifa hizo, kumemuibua Ne-yo ambaye imemlazimu kuzungumzia msiamamo wake, juu ya suala hilo hasa baada ya kujengeka kwa picha isiyo nzuri kwa upande wake kufuati kashfa hiyo nzito.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Ne-yo amesema kuwa anahitaji faragha kwenye jambo hilo, ili alishughukilikie kimya kimya, kwa kujali maslahi ya watoto wake pamoja na familia yake kwa ujumla.

Kashfa nzito inayomkabili Neyo, iliyovujishwaa na mkewe Crystal ni kuhusu mwanamuziki huyo kujihusisha na vitendo vya usaliti, kwa kutoka kimapenzi na wanawake wenye kufanya biashara ya kuuza miili yao (Machangudoa), bila kutumia kinga.

Ne-yo na mkewe Crystal Smith, katika ndoa yao wamefanikiwa kupata watoto watatu, ambao ni Shaffer mwenye umri wa miaka sita, Roman miaka mitatu pamoja na Isabella mwenye umri wa miezi 13.

Mke wa aliyeuawa huku akirekodiwa bila msaada ataka haki
Makamba aahidi mtambo wa gesi tani moja Peramiho