Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema hadi sasa hakuna chama chochote cha siasa kilicho fuata sheria na kanuni za uchaguzi za kujitoa katika uchaguzi wa marudio wa ugombea ubunge na udiwani utakao fanyika Januari mwakani

Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa mgombea wa jimbo la Singida Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), David Joseph Njumbe amekidhi vigezo vya Kikatiba na Sheria za Uchaguzi na tayari amejaza fomu zote na kuzirejesha.

Amesema kuwa kauli za viongozi wa juu wa vyama vya siasa kumkataa mgombea wao sio kazi ya tume hiyo bali na masuala ya vyama vyenyewe.

Hata hivyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema kuwa suala la vyama kujitoa katika uchaguzi ni jambo la kawaida na limekuwapo tangu chaguzi za mwanzo nchini, pia kuvikumbusha vyama vya siasa kufuata taratibu na kanuni za kuwasilisha malalamiko yao.

Video: Hatima ya Lissu, Ben Saanane hii hapa
Mwenyekiti NCCR-Mageuzi apata ajali mbaya