Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage amesema kuwa Vituo vyote vya Uchaguzi katika Uchaguzi mdogo unaofanyika hii leo vimefunguliwa kwa wakati isipokuwa kwa vituo vichache sana vilivyochelewa kwa muda wa dakika 10 kutokana na sababu za kiutaratibu.

Jaji Kaijage amesema kuwa hata hivyo zoezi hilo limeendelea katika vituo hivyo vya uchaguzi vilivyochelewa, ambapo pia ameeleza kwamba kulikuwapo na madai kuwa baadhi ya mawakala wamezuiliwa kuingia katika vituo vya uchaguzi.

Amesema kuwa katika uchaguzi mdogo wa Monduli kuna vituo 256 na ni kwenye vituo vinne tu ambapo mawakala wamekataliwa kuingia kwa sababu waliokuja si wale walioteuliwa na vyama vya siasa na kuapishwa na msimamizi wa uchaguzi.

“Walikuja mawakala mbadala wengine ambao hawakutimiza taratibu za kuapishwa na waliomba mawakala hao wanne waapishwe hapo hapo kituoni na watu ambao hawana mamlaka ya kuwaapisha,” amesema Jaji Kaijage.

Akiongea katika kituo cha Juhudi kilichopo Ukonga, Jaji Kaijage amesema jimbo la Ukonga kunavituo 673 na zoezi linaendelea vizuri, mwakala wa CCM na Chadema wapo ila mawakala wa CUF hawajaonekana na mawakala hao wamemetoa taarifa, hivyo zoezi linaendelea vizuri na hakuna changamoto ambayo iliyojitokeza.

Mapema leo, mbunge wa viti maalumu ambaye ni msimamizi wa Chadema kata ya Esilalei wilayani Monduli, Cecilia Pareso alidai kuwa mawakala wote wa Chadema kwenye kata hiyo wamezuiliwa kuingia kwenye vituo vya kupigia kura kwa kile kilichodaiwa kukosa vitambulisho vya mawakala.

Huku Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Tanzania Bara, John Mnyika akiitupia lawama Tume ya Uchaguzi ambapo amedai kuwa mawakala wake wananyanyaswa lakini wanasubiri matokeo yatangazwe ili waweze kuchukua hatua.


Video: Mgombea ajiuzulu DAKIKA 1 KABLA YA KURA KUPIGWA | Ammwagia sifa mpinzani wake hadharani

Mzee Akilimali ampasha Manara, "Nadhani bado hajaitambua ligi"
Polisi wakanusha taarifa za kushambuliwa gari la Mbunge

Comments

comments