Kamishna kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Asina Omar amefungua mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wa Uchaguzi leo Julai 30, 2020 katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ambapo amewataka wasimamizi hao kuzingatia katiba, sheria na kanuni za Uchaguzi.

Kamishna Omar amewataka wasimamizi kutoka ngazi za mikoa pamoja na majimbo kufuata taratibu zote za kikatiba na kisheri katika kusimamia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2020.

Naye Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Jacob Sifa amesimamia viapo viwili ikiwemo cha kujivua kwa uanachama wa chama cha siasa kwa wasimamizi hao na utunzaji wa siri wakati wa zoezi la uchaguzi.

Wafanyabiashara wapigwa marufuku uingizaji wa bidhaa zisizo na ubora
Maambukizi ya homa ya ini yaongezeka