Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inasubiri tangazo kwenye gazeti la serikali la kuvunjwa kwa bunge ili iweze kuweka tarehe rasmi ya uchaguzi mkuu.

Mkurugenzi wa NEC, Dkt. Wilson Mahera amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha na kusema baada ya tangazo hilo tarehe itatangazwa.

Amesema Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kifungu 37(1) kinaielekeza tume kufanya uteuzi kwa wagombea nafasi ya urais, ubunge na udiwani.

Pia ameeleza, sheria hiyo kifungu cha 46(1) kinaelekeza kuwa tarehe ya uteuzi wa wagombea itatakiwa kutajwa ndani ya siku 60 hadi 90 kabla ya kutangazwa siku ya uchaguzi.

Ndumbaro afanya ziara mipaka ya Ruvuma
Marekani: Bunge lapitisha muswada wa mageuzi idara ya polisi