Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC imeridhia kuiazima Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA sehemu ya mitambo ya TEHAMA  kwa muda wa siku 90 kwa ajili ya kuchakata taarifa wakati wa utekelezaji wa zoezi la utoaji wa vitambulisho vya taifa.

Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha tume hiyo kilichofanyika hapo jana katika ofisi za NEC jijini Dar es salaam ambapo wajumbe wamekubaliana kwa kauli moja ya kuhamishwa kwa muda mitambo hiyo kutoka ofisi zao na kwenda NIDA kwa gharama za mamlaka hiyo.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguziJaji Lubuva amesema kwamba taratibu za makabidhiano hayo zitaandaliwa ili kuwezesha mitambo  hiyo ya TEHAMA kuhamishiwa NIDA kwa muda na kufafanua kwamba kutokuwepo kwa miudombinu ya mawasiliano ambayo ingeunganisha mitambo ya NEC kwenda NIDA ndiyo sababu ya kuhamisha mitambo mahali uchakataji unapofanyika.

Aidha akiwasilisha taarifa ya wataalamu iliyopitia maombi ya NIDA Mkurugenzi wa uchaguzi  Ndg, Kailima Ramadhan amesema tume ya taifa ya uchaguzi ilinunua mitambo hiyo ya TEHAMA kwa ajili ya kufanikisha zoezi la uandikishaji wapiga kura na uchaguzi mkuu wa 2015.

Hata hivyo ameeleza kuwa mitambo hiyo ina uwezo mkubwa wa kuchakata taarifa hususani uchakataji wa alama za vidole (finger prints).

 

Meye Bastrel Kuhukumu Mchezo Wa Taifa Stars Vs Misri
Marco Reus Kuzikosa Fainali Za Euro 2016