Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeijibu Marekani na kusema kuwa zipo Sheria za kufuata iwapo kuna kasoro, baada ya Marekani kutangaza kuweka vikwazo kwa baadhi ya Maofisa wa Serikali ya Tanzania kwa madai ya kuvuruga Uchaguzi Mkuu.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amesema, taarifa hiyo haijafafanua kinacholalamikiwa na sheria  za Tanzania zinaelekeza kupeleka mashtaka Mahakamani pale mlalamikaji anapoona Sheria hazikufuatwa.

Jaji Kaijage amesema katika Uchaguzi huo kulikuwa na waangalizi na walitoa ripoti zao za awali na wameendelea kutoa ripoti kuu.

“Unaposema Uchaguzi umeingiliwa inakuwa ni ‘general statement’. Ni lazima useme umeingiliwa kivipi? sio ‘sweeping statement’. Sheria zetu ziko wazi kama unaona kuna kasoro baada ya Uchaguzi unafanya uchunguzi wa kisheria na unakwenda Mahakamani kushitaki” amefafanua Kaijage.

Tanzia: Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma afariki dunia
Tanzia: Mbunge wa viti maalum afariki dunia