Wafuasi wa vyama vinavyounda Ukawa leo wamepata habari njema baada ya siku moja ya sintofahamu kufuatia uamuzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwazuia kutumia uwanja wa Jangwani kwa uzinduzi wa Kampeni zao, Jumamosi hii.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mkuu wa idara ya mawasiliano ya Chadema, Bw. Tumaini Makene, vyama hivyo vitafanya mkutano wa uzinduzi wa kampeni zao katika uwanja huo kama ilivyopangwa awali baada ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa kuingilia kati na kutengua uamuzi wa Manispaa ya Ilala.

Viongozi wa Ukawa wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwakemea watumishi wa umma kufanya kile walichodai kuwa ni kutumia nafasi zao kufanya kazi za chama tawala na kuvibana vyama vingine pale vinapohitaji huduma zao kwa mujibu wa sheria.

Jana, viongozi wa Ukawa walipokea barua kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ikitaarifu kuwa ombi lao la kutumia uwanja wa Jangwani, Dar es Salaam Jumamosi hii kuwa limekataliwa kwa kuwa uwanja huo tayari umeshalipiwa na mtu mwingine.

Miss Tanzania Yatangaza Kamati Mpya, Jokate Apewa Shavu
‘Helkopta’ Rukhsa Kunogesha Kampeni