Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) imerejesha Serikalini kiasi cha shilingi bilioni 12 zilizobaki katika bajeti ya Uchaguzi Mkuu uliopita.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva na Mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume hiyo, Ramadhani Kailima leo wamemkabidhi Rais Magufuli mfano wa hundi yenye kiasi hicho cha fedha zilizobaki, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Miezi kadhaa iliyopita, Ofisi ya Bunge ilimkabidhi Rais John Magufuli kiasi cha shilingi bilioni 6, fedha ambazo aliagiza zitumike kwa ajili ya kutengeneza madawati ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Rais Magufuli amteua Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu
TFF Yatangaza Kozi Za Ukocha