Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu, Semistocles Kaijage  amewataka wasimazi wote wa uchaguzi kufuata maadili na kuzingatia maelekezo waliyopewa.

Amesema hayo wakati akizungumza na vyama vya siasa ambapo tayari wasimamizi wa uchaguzi wameshateuliwa  na wanaendelea na mafunzo ambayo yatakamilika Jumatatu Agosti 03, 2020.

“Tayari tumekutana na wasimamizi wote wa uchaguzi upande wa Tanzania Bara Julai 24, 2020 jijini Dodoma na msisitizo uliowekwa wazingatie maadili ya uchaguzi na maelekezo yanayotolewa na NEC” Amesema Jaji Kaijage.

Pia amesisitiza watendaji wa uchaguzi wanatakiwa kuwepo kwenye ofisi na atakayekiuka ni kinyume cha maadili na hawatakubali kitendo hicho.

Arteta atamani mafanikio ya Chelsea
Coastal Union yazionya Simba SC, Young Africans