Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC), imekubali rufaa 15 kati ya 55 za wagombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu na kuwarejesha katika orodha ya wagombea.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa NEC Dkt. Wilson Mahera, leo Septemba 8 2020, imeeleza kuwa NEC imekataa rufaa 15 za wagombea ambao hawakuteuliwa.

Dkt. Mahera amesema tume hiyo baada ya kuchambua rufaa hizo kupitia vielelezo mbalimbali rufaa 25 za kupinga kuteuliwa.

Aidha, amesema wahusika wa rufaa hizo wameanza kupokea uamuzikwa njia za barua na tume inaendelea kupitia rufaa zote na watatoa taarifa kadri wanavyomaliza kuzishughulikia.

Mwamba amerudi, kupambania taji 2020/21
TMA: Pandeni mbegu za muda mfupi