Hatimaye Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) imeweka wazi idadi ya wabunge wa viti maalum ambao vyama vya siasa vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu vimepata kulingana na idadi ya wabunge wake wa kuchaguliwa.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva, jana alieleza kuwa taratibu za mgawanyo wa nafasi za ubunge wa viti maalum zimekamilika huku nafasi tatu zikiwa zimebaki kutokana na majimbo nane yanayosubiria kufanya uchaguzi wa Ubunge kutokana na vifo vya wagombea.

Bungeni Dodoma

Kwa mujibu wa NEC, Chama cha Mapinduzi kimeweza kupata nafasi ya wabunge 64 wa viti maalum huku Chadema wakijipatia viti 36 na CUF viti 10. Idadi hiyo inaonesha kuwepo ongezeko kubwa la wabunge wa vyama vya upinzani katika bunge la 11 ukilinganisha na ilivyokuwa katika Bunge la 10.

Rais John Magufuli tayari ameitisha kikao cha kwanza cha Bunge la Kumi na Moja, November 17 na November 19 mwaka huu ambapo atapendekeza jina la Waziri Mkuu.

Wapinzani Zanzibar Wagawanyika
Polisi Wabainisha Uhalifu Uliofanywa Na Kituo Cha Sheria, Haki Za Binadamu ‘LHRC’