Leo Julai 13, 2018 Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), limetangaza matokeo ya kidato cha sita ambapo limetaja shule zilizofanya vizuri na shule zilizoshika mkia katika mitihani huo.

Ambapo imetaja shule ya Kibaha, Kisimiri, kemebos na Mzumbe, kuibuka kidedea katika shule zilifanya vizuri shule nyingine zilizoshika kumi bora, ni Feza Boy’s, Marian Boys, Ahmes, St Mar’ys Mazinde Juu, Marian Girls na Feza Girls’s.

Necta pia imeweka bayana shule zilizoshika mkia katika mitihani hiyo zikiwemo, shule ya Forest (Morogoro), Jang’ombe, St. James, Kilolo (Iringa), White lake (Dar es salaam), Aggrey (Mbeya), Nyaligamba (Kagera), Musoma Utalii, (Mara), Ben Bella, (Mjini Magharibi) na Golde Ridge (Geita).

Ubora wa ufaulu kwa watahiniwa wa shule umeonesha kuwa jumla ya watahiniwa 72,866 sawa na asilimia 95.52 wamefaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu wakiwemo wasichana 30,619 sawa na asilimia 95.92 na wavulana 42,247 sawa na asilimia 95.23. jumla ya watahiniwa wote waliopata daraja la kwanza ni 8,168 ikiwa ni jumla ya wavulana 5,153 na wasichana 3,015.

Matokeo hayo yametangazwa na Katibu Mkuu Mtendaji NECTA, Charles Msonde akiwa mjini Zanzibar.

Aidha jumla ya watahiniwa 83,581 sawa na asilimia 97.58 ya watahiniwa 86,105 waliofanya mtihani wa kidato cha sita mwezi Mei, 2018 wamefaulu na ufaulu huo ni sawa na ongezeko la asilimia 1.53 kutoka asilimia 96.06 mwaka jana, 2017.

Ubunifu wa Veta, bodaboda kutowaka bila kuvaa ‘helmet’
Video: Kiongozi NCCR Mageuzi akimbilia CCM, afunguka madudu ya upinzani