Mwimbaji Nedy Music amesema hajutii kujiunga na lebo ya Pozi kwa Pozi (PKP) inayomilikiwa na Ommy Dimpoz kama baadhi ya watu wanavyodai.

Msanii huyo amesema amepata faida ya aina yake tangu alipoanza kufanya kazi chini ya Ommy Dimpoz tofauti na alivyokuwa akifanya kazi mwenyewe.

Amesema faida kubwa aliyoipata sio pesa au mali bali ni watu aliokutanishwa nao tangu ajiunge na PKP.

“Faida kubwa niliyoipata tangu kujiunga PKP nikukutanishwa na watu tofauti ambao nilikuwa natamani muda mrefu kukutana nao,” Nedy ameiambia BongoDotHome ya 100.5 Times Fm.

“Unajua mtu akikukutanisha na watu kwa sababu zake hata kama kesho hayupo ile connection inabaki, ameongeza.

Ney Wa Mitego ajifananisha na Juma Nature

Katika hatua nyingine, msanii huyo amezungumzia hali ya Bosi wake Ommy Dimpoz kujiunga na lebo ya Rockstar4000.

Janjaro azungumzia mpango wa kutaka kujiunga na ‘Weusi’

Amesema hatua hiyo haijaathiri utendaji wao wa kazi na anaamini kuna mazuri kutoka katika lebo hiyo kubwa yatakuwa yakimfikia.

“Haijaathari kitu chochote kwasababu  mimi nipo chini ya Ommy na nadhani kuna vitu vizuri kutoka  Rockstar4000 vikashuka mpaka kwangu,” amesema Nedy music.

Nash Mc awasili Uganda kuiwakilisha Tanzania katika sanaa na Hip Hop
Wanajeshi waua watu wanane kwenye maandamano ya ‘uhuru’