Mbunge wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe, Neema Mgaya amesema kuwa anapinga vikali mauaji ya watoto wadogo mkoani humo na kwamba matukio hayo ya kinyama hayavumiliki.

Ameyasema hayo mkoani humo wakati akitoa pole kwenye msiba wa mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Matembwe, Tarafa ya Lupembe Wilayani Njombe, Rachel Malekela(7) aliyefariki dunia kwa kuchinjwa na kutupwa kichakani ikiwa ni hatua chake kufika nyumbani na watu wasiojulikana .

Amesema kuwa matukio hayo yanapaswa kupingwa vikali kwani yanakatisha uhai wa watoto ambao ni taifa la kesho.

‘’Napiga vita vikali huu unyama wanaofanyiwa watotot wetu katika mkoa huu wa Njombe, inasikitisha sana, Mimi ni mama nina zungumza haya kwa uchungu wanawaua watoto kikatili kwani wamekosa nini, Njombe mambo haya hatuna yametoka wapi inashangaza sana,’’amesema Mbunge huyo.

Aidha, amewataka wananchi wa mkoa wa Njombe kushirikina na vyombo vya usalama kwa kuhakikisha wanatoa taarifa za awali ili ziweze kufuatilia kwa karibu na kuweza kuwakamata wahalifu.

Hata hivyo, Mauaji hayo ya kutatanisha yamefikia idadi ya watoto wa saba kukutwa wamefariki na miili yao kutelekezwa katika misitu

Tukumbushane tafsiri 4 za kumpa mwenza wako zawadi
Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani wamjibu Tundu Lissu