Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznania Dkt. Isdory Philip Mpango leo Julai 26, 2021 ataweka jiwe la Msingi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini Mtwara ikiwa ni sehemu ya ziara yake.

Aidha Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa maandalizi ya shughuli ya uwekaji jiwe la msingi katika Hospitali hiyo yamekamilika kwa asilimia 100.

Ujenzi wa Hospitali hiyo unasimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi chini ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC ambapo hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 97.

Naibu Waziri Wizara ya Afya Mollel amesema Kukamilika na kuanza kwa huduma za tiba katika Hospitali hiyo kutapunguza adha kwa wananchi wa Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kusafiri umbali mrefu kwenda kupata huduma za matibabu ya kibingwa.

Rais avunja Bunge, kumtimua Waziri Mkuu
PICHA: Mabingwa ASFC waanza safari ya Dar es salaam