Klabu ya Manchester United imempatia Ofa ya Mkataba mpya Kiungo wa Kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba wenye thamani ya kitita Cha £500,000 kwa wiki na kumfanya Nyota Huyo Kuwa Mchezaji anayelipwa Fedha Nyingi zaidi Katika Ligi Kuu ya England

Pogba anayeuguza Majeraha anataraji kurejea Uwanjani Mwishoni mwa Mwezi Januari naikumbukwe kuwa Msimu Huu wa mwaka 2021/2022 Kiungo Huyo ameitumikia Manchester United Katika Michezo 9 na Kutoa pasi “Assist” 7 zilizozaa Mabao

Mkataba wa Pogba unamalizika mwishoni mwa Msimu huu, Ofa Hiyo Imekuja ikiwa Ni Siku Chache baada ya Klabu ya Manchester United kumtambulisha Afisa mtendaji Mkuu mpya bwana Richard Arnold anayetaraji Kuanza Majukumu Yake mapema Mwezi Februari.

Simba SC yatoa onyo kali Jezi Feki
Trippier akaribishwa Newcastle UTD