Ikiwa ni muendelezo wa kukuza urafiki wa China na Tanzania kampuni zaidi ya 100 kutoka china zinatarajia kukutana na wanafunzi wanaotarajiwa kumaliza vyuo nchini mwaka huu  kujadili kupunguza tatizo la ajira kwa wahitimu watarajiwa mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam  Upande wa Taaluma, Prof.Florence Luhoga amesema wameamua  kuwakutanisha wawekezaji hao pamoja na wanafunzi wahitimu watarajiwa wa vyuo vikuu mbalimbali Tanzania ili kuweza kubaini wenyewe mahitaji yao ya wafanyakazi wazawa.

Mkusanyiko wa Kampuni hizo ni moja ya juhudi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Confucius ya Chuo hicho na Jumuiya ya wafanyabiashara wa China Tanzania za kupunguza tatizo la ajira kwa wahitimu watarajiwa ambapo tatizo hilo limezidi kuwa tatizo kubwa nchini.

aidha Prof Luhoga amesema “Hii ni fursa kwa Watanzania hasa wale wahitimu watarajiwa kwenye vyuo vyetu, lakini pia nifursa kwa wanafunzi hivyo ni muhimu siku hiyo wakaja na vyeti vyao halisi na CV zao kwasababu kutakuwa na kampuni zitakazowafanyia usahili papo hapo.”

Aidha Luhoga amevitaja vyuo vinavyoshiriki moja kwa moja kwenye maonyesho hayo ya kazi za kampuni kuwa ni, Mwalimu JK.Nyere ya kampasi  Dar es Salaam, Chuo Kiuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Kampasi ya Elimu (DUCE), Chuo cha Mkwawa (MUSE) na Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST), Chuo Kikuu chaSt.Augustine (SAUTI), Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Chuo Kikuu cha Dodoma huku zaidi ya wahitimu 5000 wanatarajiwa kushiriki.
Pamoja na hayo malengo ya kampni hizo ni pamoja na kuimarisha uhusiana baina ya Tanzania na China pia kuisaidia serikali  mpya kupunguza vijana wanaokosa ajira pindi wamalizapo vyuo na kusaidia makampuni ya china kuwekeza nchini.
Maonyesho hayo ya kazi za kampuni yanatarajiwa kujikita katika taaluma za Biashara, Rasilimali watu,utunzaji wa kumbukumbu, Uongozi katika Biashara, Uhandisi wa aina mbalimbali na fani zingine mbalimbali,
Hii ni mara ya kwanza kuandaliwa kwa mkusanyiko huo na unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii na kutoa fursa kubwa ya ajira za ndani ya nchi na pamoja na nchini  China kwa wanafunzi watakao fuzu kwenye usaili.
Rais Magufuli amemteua Prof. Rubaratuka kuwa Mwenyekiti TPA
Mtanzania Jasper Makala aibuka kidedea tena Washington DC-USA