Shirikisho la soka nchini TFF limetimiza ahadi ya kuifanyia marekebisho Ngao ya Jamii ambayo ilizua mjadala miongoni mwa wadau wa soka nchini kuputia mitandao ya kijamiii, kutokana na neno la SHIELD kukosewa wakati ikikabidhiwa kwa washindi wa mchezo wa Ngao ya Jamii mwaka 2017, Wekundu wa Msimba Simba.

Neno SHIELD katika Ngao hiyo lilikosewa na kuandikwa SHEILD hali ambayo iliilazimu sekretarieti ya shirikisho la soka nchini TFF kuutaka uongozi wa klabu ya Simba kuirudisha ili ikafanyiwe marekebisho, huku ikisemekana baadhi ya wahusika waliwajibishwa kwa kosa hilo.

Afisa habari wa TFF Alfred Lucas mapema hii leo aliionyesha Ngao ya Jamii katika mkutano na waandishi wa habari, kwa lengo la kuthibitisha marekebisho yaliyofanywa, huku akiahidi ngao hiyo itakabidhiwa kwa wahusika kabla ya mchezo wa mzunguuko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Septemba 06 dhidi ya Azam FC.

Hata hivyo tatizo la kukosewa kwa neno SHIELD bado lipo kwenye nishani walizopatiwa wachezaji na viongozi wa Young Africans na Simba SC.

Mbao FC Yapata Mdhamini Mpya
Lissu aungwa mkono na Kituo cha Haki za Binadamu LHRC