Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amelisifu jeshi lake kufuatia mauaji ya Wapalestina 17 katika mpaka wa Gaza, wakati ambapo jumuiya za kimataifa zikilaani mauaji hayo.

Katika taarifa yake aliyoitoa Jumamosi, Netanyahu amevishukuru vikosi vyake kwa kile alichokiita ‘kulinda mipaka ya nchi hiyo’ na kisha kuwaruhusu Waisrael kusherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa amani.

“Kazi nzuri wamefanya wanajeshi wetu,” alisema.

Maelfu ya Wapalestina waliandamana katika eneo la Gaza, siku ya Ijumaa ambapo mbali na vifo vya watu 17, watu 1,500 kati yao walijeruhiwa baada ya wanajeshi wa Israel kufyatua sisasi.

“Nalaani vikali Serikali ya Israel kufanya mashambulizi kinyume cha haki za binadamu,” amesema rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan katika hotuba yake ya Jumamosi kwa taifa lake.

Nayo Qatar ililaani vikali kitendo hicho na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kwa dharura kujadili tukio hilo.

Viongozi Chadema kusherekea Pasaka Gerezani
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 1, 2018