Nahodha na Beki wa pembeni wa zamani wa Manchester United Gary Neville, amesema klabu hiyo haina ubavu wa kutwaa taji la Ligi Kuu England (EPL) msimu huu, kutoka mikononi mwa mahasimu wao Manchester City.

Neville ambaye aling’ara wakati wa utawala wa meneja Sir Alex Ferguson ameyasema hayo, kufuatia kuchoshwa na mwenendo wa kikosi cha klabu hiyo, ambayo msimu huu inapewa nafasi kubwa ya kumaliza kiu ya ubingwa wa England.

Amesema sio muda sahihi kwa wadau wa soka duniani kuanza kuifikiria Manchester United kwenye mbio za ubingwa, na badala yake wanapaswa kuungana ili kuushinikiza Uongozi uweze kumuondoa Ole Gunnar Solkajaer, ambaye amedai ameshindwa kufanya kazi yake ipasavyo tangu alipokabidhiwa majukumu ya kuliongoza benchi la ufundi la klabu hiyo.

Wakati akipendekeza kuondolewa kwa meneja huyo kutoka nchini Norway, Neville ameutaka uongozi wa Manchester United kumfikiria meneja kutoka nchini Italia Antonio Conte, ili wamkabidhi mikoba ya kuwa mkuu wa benchi la ufundi klabuni hapo.

Mwishoni mwa juma lililopita Manchester United ilipoteza nyumbani dhidi ya Aston Villa kwa kufungwa bao moja kwa sifuri katika mchezo wa Ligi Kuu ya England, lakini jana Jumatano (Septamba 29) ilirejea katika ushindi kwa kuifunga Villareal mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani ulaya.

Kijaji:ALAT tekelezini haraka mfumo wa Anuani za makazi
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 30, 2021