Kiungo kutoka nchini England na klabu ya Swansea City, Jonjo Shelvey anaamini mchezo wa kombe la FA uliowakutanisha dhidi ya Oxford United, huenda ukawa wa mwisho kwake msimu huu.

Njonjo, anaamini hivyo kutokana na tetesi zinaendelea kushika kasi dhidi yake ambazo zinadai yu njiani kusajiliwa na klabu ya Newcastle Utd katika kipindi hiki cha majira ya baridi (Dirisha dogo la usajili)

Meneja wa klabu ya Newcastle Utd, Steve McClaren, anatajwa kuwa katika mipango madhubuti ya kutaka kumsajili kiungo huyo kwa ada ya uhamisho wa paund million 10, huku akiAmini huenda akawa suluhisho katika kikosi chake katika kipindi hiki.

Hata hivyo, bado mazungumzo ya usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 hayajaanza, japo tetesi za uhamisho wake zinaendelea kushika kasi siku hadi siku.

Jonjo Shelvey was given abuse from the standsJonjo Shelvey akijibishana na shabiki aliyekereka na matokeo ya jana dhidi ya Oxford United

Inaaminiwa huenda Shelvey anajua kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka Liberty Stadium, hali ambayo inatajwa ilimsukuma kuonyesha utovu wa nidhamu mara baada ya mchezo wa kombe la FA hapo jana, kwa kumuonyesha ishara ya matusi shabiki aliyekua akilalamikia matokeo ya kufungwa mabao matatu kwa mawili.

Alipoulizwa meneja wa Swansea City, Alan Curtis juu ya utovu huo wa nidhamu alisema hakuona kitendo hicho.

Tuchel: Aubameyang Hauzwi Kwa Gharama Yoyote
Dakika 180 Za Vita Azam FC Ligi Kuu