Ney wa Mitego amesema kuwa hana kumbukumbu ya kufanya shows katika bara la Ulaya kama ilivyo kwa wasanii wengine kwa kuwa hukataa mialiko mingi anayopewa kwakuwa mapromota wa nchi hizo huwalipa wasanii wa Tanzania kiasi kidogo sana cha fedha kisichofikia kiwango wanacholipwa nchini.

Msanii huyo alikiambia kipindi cha Ubaoni cha E-FM jana kuwa ukiwaacha Diamond na AY, wasanii wote wa Bongo Flava wanaofanya shows barani Ulaya hulipwa kiwango kisichozidi $500 hadi $1,000 (sawa na shilingi za Tanzania 1,094,350 hadi 2,188,700).

“Siwezi kwenda Ulaya kwa sababu ya kupata picha za kupost Instagram halafu nikaacha watoto wangu wanakufa njaa. Jana nilipokea show ya Italy, lakini hawalipi vizuri. Anaelipwa vizuri labda ni mmoja au wawili ambao ni Diamond na AY,” alisema

Nay wa Mitego alimrushia kijembe kingine Ommy Dimpoz ambaye aliwahi kudai kuwa Nay ni mshamba kwakuwa hana historia ya kwenda Ulaya mara nyingi kama yeye.

“Ommy ni mshikaji wangu, mimi na yeye hatuna ugomvi, lakini naliongea tu hili… kwa kweli Ommy navyomuelewa anavyopenda sifa, akafanya show Ulaya ikapiga nyomi ya kueleweka asiposti Instagram?” Alihoji. “Wewe ulsihawahi kumuona Ommy amepost show yake yoyote ya Ulaya? au anapigia uwani?”

 

 

Matokea kidato cha 4: ‘Mchina’ ayeshika nafasi ya pili kitaifa afunika Kiswahili, aliyeongoza aiota Harvard
Magufuli ageukia wasanii, aagiza TRA kufanya operesheni kama ya makontena