Rapa  Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameweka wazi sababu zinazofanya  vijana wengi kushindwa kufikia malengo yao na amewapa njia za wao kupita ili kufikia mafanikio makubwa katika maisha.

Akizungumza Dar es salaam jana, Nay alisema vijana wengi wanashindwa kufanikiwa kutokana na ukweli kwamba hawajitambui na hawajui wanataka nini huku wengine wakiendekeza sana starehe kuliko hata kipato chao.

”Unajua ukitaka kufanikiwa katika jambo lolote kwanza lazima ujitambue, ujue unataka nini, wapi unataka kufika na utafikaje hapo, tatizo vijana wengi siku hizi hawajitambui lakini pia tunakuwa na kampani za watu ambao si watu sahihi naweza kusema kampani ambazo si rafiki na ndoto zako’,” alisema Ney wa Mitego

Aliendelea kwa kusema ”unaweza kujikuta unakuwa na kampani ya watu wanaopenda sana starehe kuvaa sana pasipo kuwa na malengo mwisho wa siku unashindwa kufikia ndoto zako,”.

Ili mtu afanikiwe katika maisha na kuwa na maisha mazuri lazima ajitambue na kupunguza marafiki ambao  hawana msaada katika maisha kwake, watu ambao wanaweza kumrudisha nyuma na anapaswa kuwa na urafiki na watu ambao wanaweza kumsaidia kufikia malengo yake, alisema Ney wa Mitego.

Sanamu ya Lionell Messi yavunjwa
Nape Nnauye afanya uteuzi

Comments

comments