Mwanamuziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki, alimaarufu kama Ney wa Mitego amesema yeye ndio chanzo cha maamuzi ya nyimbo 15 za bongo fleva kufungiwa ikiwa pamoja na nyimbo zake tatu, ambazo ni Mikono juu, Makuzi na Pale kati, hivyo amesema anajiona akiacha kufanya kazi hiyo ya muziki na kujihusisha na shughuli nyingine.

Nyimbo hizo zilitangazwa na Mamlaka ya Mawasiliano kupigwa marufuku kuchezwa katika vituo vya habari nchini kwa kuwa hazijazingatia maadili ya Tanzania na kuvunja baadhi ya vifungu vya sheria za taaluma hiyo.

Ney amesema ”Sioni nikibadilisha mfumo wa mashairi kwa sababu nitakuwa nimeenda kuharibu sanaa yangu, labda najiona nikienda kuacha kazi ya muziki na kuamua kufanya shughuli nyingine”. amesema Ney wa mitego.

Ameongezea ‘Wakati mwingine naona kuwa sababu ya kufungiwa kwa miziki hii ni mimi na wengine wanawekwa kama chambo kwa kuwa kati ya nyimbo zote hizo,  nyimbo mpya ni yangu tu ambayo imetoka wiki mbili zilizopita na video ina wiki moja tu” Ney wa Mitego.

Ney amezungumza hayo alipohojiwa na Chombo cha habari cha BBC Swahili, kufuatia na orodha iliyotolewa na Basata huku nyimbo zake tatu kufungiwa ikiwemo nyimbo yake mpya aliyoitoa wiki mbili iliyopita.

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa mwanamuziki huyo kupata misukosuko katika muziki wake.

Mnamo mwezi machi mwaka jana Ney wa Mitego aliwahi kukamatwa na jeshi la polisi la Tanzania kwa kosa la kuimba wimbo unaokashifu serikali lakini inakumbukwa kuwa mwanamuziki huyo aliwahi kupewa onyo kuhusiana na mavazi yake.

 

 

Chin Bees kuzindua album yake leo, kutoa nakala bure kwa mashabiki
Madaktari bingwa waleta mgomo