Mahasimu wa mjini Mannchester nchini England, Manchester United na Manchester City wameingia katika vita kubwa ya usajili unaomlenga mshambuliaji hatari kutoka nchini Brazil na klabu ya FC Barcelona ya nchini Hispania, Neymar.

Baba wa mshambuliaji huyo amekua wa kwanza kuweka hadharani vita hiyo ya usajili wa mwanae, baada ya kutangaza muelekeo wa Neymar kuwa mbioni kuondoka FC Barcelona.

Baba Neymar, amesema kwa sasa mwanae hana sababu ya kuboresha mkataba wake, mara tu, utakapofikia kikomo mwaka 2018.

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la The Sun, klabu hizo za Manchester zinajiandaa kufikia dau la pauni million 144, ili kuweza kupata huduma ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24.

Klabu zote mbili pia zimetajwa kuwa tayari kumlipa mshahara Neymar wa Paund million moja kwa juma, ambapo ofa hiyo itamfanya mshambuliaji huyo kuwa mwanasoka ghali zaidi duniani, ingawa hilo halichukuliwi kama kishawishi cha kumuwezesha kuiacha FC Barcelona.

Hata hivyo, kama Neymar atashawishika kuondoka FC Barcelona, klabu ya Man City ndio inayopewa nafasi kubwa ya kumtia mikononi kutokana na ujio wa meneja kutoka nchini Hispania Pep Guardiola.

Neymar aliwahi kukaririwa akisema, angependa kufanya kazi na meneja huyo.

Liverpool Yaingia Katika Vita Ya Kumuwania Chicharito
Shilole awahubiri mabinti