Mshambuliaji kutoka Brazil na klabu Bingwa nchini Ufaransa PSG, Neymar da Silva Santos Júnior anafikiria kuondoka klabuni hapo msimu huu wa usajili wa majira ya kiangazi, baada ya kugundua kuwa Uongozi wa klabu hautajali endapo ataondoka.

Klabu ya Chelsea ya England, inatajwa kuwa klabu pekee iliyoonesha nia ya kutaka kumsajili Mshambuliaji huyo, kufuatia mmiliki wake mpya Todd Boehly kutoa kauli kubwa katika soko la usajili msimu huu wa usajili wa majira ya kiangazi.

Mbali na taarifa hizo, pia Beki wa Chelsea ambaye ni Raia wa Brazil na rafiki wa karibu wa Neymar, Thiago Silva amethibitisha kufanya mazungumzo na Mshambuliaji huyo, na kuonesha nia yake ya kutaka kucheza soka jijini London (Stamford Bridge).  

Hata hivyo, inabakia kuonekana ikiwa Chelsea na Thomas Tuchel wana nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, itathibitika baadae kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili nchini England.

Neymar alisaini mkataba mpya na PSG miezi 12 iliyopita, na mshahara wake kwa kila mwaka ni Euro milioni 43 bila bonasi, amebakiza miaka mitano katika mkataba huo.

Mashindano utamaduni kuanzia ngazi ya kata
Issa Ndala mali halali Azam FC