Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar, 25, ameruhusiwa kufanya mazungumza rasmi kuhusu uhamisho wake wa rekodi ya dunia wa pauni milioni 198 kwenda katika Klabu ya Paris St-Germain ya nchini Ufaransa.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil aliwaambia wachezaji wenzake siku ya Jumatano kuwa anataka kuondoka Barcelona kwenda kujiunga na Klabu hiyo ya matajiri yenye maskani yake jijini Paris, Ufaransa .

Aidha, Neymar amepewa ruhusa hiyo ya kwenda kufanya mazungumzo na meneja wake, Ernesto Valverde ya kutokwenda mazoezini badala yake akashughulikie mpango wake wa uhamimisho.

Hata hivyo, Mkataba wa Neymar una kifungu cha Euro milioni 222 ambacho PSG wapo tayari kukitengua ili kuweza kukamilisha usajili huo wa mwanasoka huyo kijana na mahiri kutoka nchini Brazil.

 

Video: CCM inalinga tu kwa sababu inabebwa na dola-Sumaye
Video: Goodluck Gozbert atoa mpya nguvu ya 'shukrani'