Wachezaji wa timu ya Barcelona wako tayari kucheleweshewa kulipwa mshahara ikiwa hatua hiyo itasaidia klabu hiyo kumsajili tena mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil, Neymar Santos msimu wa joto.

Akiongea na kituo kimoja cha redio nchini Hispania kinachofahamika kwa jina la Cadena Ser, mchezaji wa timu hiyo, Gerard Pique amesema wachezaji wenzake waliiambia klabu hiyo kuwa wako tayari kuchelewa kulipwa mishahara ili kuisadia kufikia kanuni ya timu ya malipo sawa ya wachezaji.

“Tuko tayari kandarasi zetu zifanyiwe marekebisho, hatuna mpango wa kuchanga pesa, lakini tutarahisisha mambo kwa kuruhusu baadhi ya malipo kutekelezwa katika mwaka wa pili au watatu badala ya mwaka wa kwanza.”

Barcelona ilitumia zaidi ya £200m msimu wa joto, katika usajili wa wachezaji kama Frenkie de Jong, kiungo wa kati kutoka Ajax na Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid.

Inasadikiwa kuwa moja ya suala ambalo Barcelona inatakiwa kushughulikia kabla ya kumsaini Neymar ni kanuni ya malipo sawa ya wachezaji ambayo inazuia vilabu kutumia fedha kuliko uwezo wao

Neymar aliondoka Barcelona na kujiunga na Paris St-Germain kwa ada ya kuvunja rekodi duniani ya euro milioni 222 mwaka 2017.

 

Prof. Kilangi awataka wanasheria wa serikali kubadilika ''Jamii itawabadilisha''
Video: Jurgen klopp azua balaa Uingereza, agoma kuipeleka Liverpool uwanjani

Comments

comments