Mchezaji wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Neymar da Silva Santos amezungumzia uamuzi wa mpachika mabao mwenzake, Lionel Messi kung’atuka kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina.

Messi alitangaza uamuzi wake wa kuacha kuichezea timu yake ya taifa baada ya kushindwa kubeba ndoo mara tatu ‘mfululizo’ katika mashindano makubwa licha ya kuingia fainali. Mwaka huu ikiwa imepoteza dhidi ya Chile katika fainali za Copa America.

Neymar amesema kuwa uamuzi huo wa swahiba wake Messi ambaye ametwaa mara tano tuzo za mwanasoka bora wa kiume wa dunia za Ballon d’Or, ni pigo kwa mpira wa miguu duniani. Alienda mbali na kueleza kuwa anaamini bila Messi mpira wa miguu hautakuwa kama ulivyo.

“Ninaheshimu uamuzi wake wa kustaafu, lakini mpira wa miguu bila Messi sio mpira wa miguu, ni ngumu kuvuta hiyo taswira bila yeye,” Neymar aliiambia Marca.

“Kama unapenda soka kwa namna yoyote, huwezi kuficha bali kumkubali Messi na kila mafanikio aliyofikia akiwa na Argentina na Barcelona,” aliongeza.

Hivi karibuni, Messi amekumbwa na janga la kuhukumiwa kifungo cha miezi 21 jela kwa kosa la ufisadi katika kodi.

Mourinho ang’oa ‘hirizi’ za Van Gaal uwanja wa mazoezi, apachikwa jina jipya
Shule ya Sekondari Lindi Yaungua Moto