Mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona, Neymar da Silva Santos Júnior, amelazimika kuomba radhi kufuatia ujumbe aliouandika katika mtandao wa Instagram, na kusababisha mkanganyiko kufuatia kutupwa nje kwa timu ya taifa ya Brazil kwenye michuano ya Copa America kwa kufungwa na Peru.

Saa kadhaa baada ya mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita na kushuhudia Brazil wakifungwa bao moja kwa sifuri, Neymar aliweka picha sambamba na ujumbe wa maneno katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram uliosomeka kwamba, “anajivunia kuvaa jezi ya Brazil na kwamba baada ya tukio hili mengi yatazungumzwa”.

Ujumbe na picha hiyo vilipokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wake ambao wanamfuata kwenye ukurasa wa Instagram wanaokaribia milioni 51.

Kutokana na hatua hiyo, mshambuluaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ameomba radhi kwa lugha ya kuudhi aliyoitumia.

“Dakika tano Brazil zilitosha kuona kwamba posti yangu Instagram haikuwa na lengo tofauti,” Neymar aliandika. “Nilichokisikia kutoka kwa watu niliokutana nao uwanja wa ndege sijawahi kufanya, nakiri ndio nilitazama tofauti, naomba radhi kwa wote niliowakwaza.”

“Niliandika baada ya matokeo ya Brazil na Peru na niliumia sana nikasukumwa kuandika nilivyoandika, mimi ni sehemu ya timu ile.”

Video: CUF Dar kufanya maandamano kumuunga mkono Profesa Lipumba
Robert Emmanuel Pirès Amshurutisha Jamie Vardy