Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Neymar da Silva Santos Júnior, anataka kumaliza soka lake akiwa na Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain ‘PSG’, licha ya rekodi kutokuwa rafiki kwake kulingana na namna ambavyo mastaa wenzake wa Kibrazili walivyoachana na soka la Ulaya mapema.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na miamba hiyo ya Ligue 1 mwaka 2017 kwa dau la Rekodi la Pauni Milioni 200, na amekuwa sehemu muhimu timu ya PSG kushinda mataji manne ya ligi katika kipindi hicho.

Hata hivyo, haujawa mwezi mzuri kwa Neymar, kwani kwa sasa yuko nje anatakosekana kikosini hadi mwishoni mwa msimu huu kutokana na kuumia kifundo cha mguu.

Uongozi wa klabu ya PSG uliona matumaini yao ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu yalimalizwa kwa kufungwa jumla ya mabao 3-0 na Mabingwa wa Ujerumani FC Bayern Munich Jumatano iliyopita.

Licha ya matatizo ya PSG ya ndani na nje ya Uwanja, na uvumi wa mabadiliko makubwa katika klabu hiyo msimu ujao ili kuhakikisha wanakuwa na Wachezaji watakaopambana kwa kiasi kikubwa ili kubeba Ubingwa wa Ulaya, inadaiwa Neymar amejitolea kuendelea kusalia Paris.

Mbrazil huyo alisajiliwa PSG akitokea FC Barcelona miaka sita iliyopita, kwa mkataba wa Rekodi ya Dunia wa Pauni Milioni 200 na uwepo wake klabuni hapo umewasaidia kuongeza thamani yao hadi kufikia Pauni bilioni 2.7.

Mameya miji 50 wajadili utatuzi magonjwa yasiyoambukiza
Kigogo afumaniwa na dada wa kazi, akimbia