Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain ‘PSG’ mwishoni mwa msimu huu 2022/23, huenda wakaachana na Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Neymar da Silva Santos Júnior.

Msukumo wa kuachwa kwa Mshambuliaji huyo unatoka kwa Mkurugezi wa Ufundi wa PSG Luis Ocampos, ambaye amedhamiria kufanya mabadiliko kwenye kikosi, ili kumpata mshambuliaji mpya.

Taarifa kutoka jijini Paris zinaeleza kuwa tayari Luis Ocampos, ameshakabidhiwa majina matatu ya Washambuliaji, ambapo mmoja wao anapaswa kutua klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Watatu hao wanaotajwa kuwaniwa na PSG ni Marcus Rashford (Manchester United), Rafael Leao (AC Milan) na Victor Osimhen (SSC Napoli).

Neymar aliyesajiliwa klabuni hapo mwaka 2017, na tayari ameshaitumikia Paris Saint-Germain katika michezo 110 na kufunga mabao 81.

PSG ilimsajili Neymar akitokea FC Barcelona kwa ada ya Euro Milioni 222.

Sina kinyongo na yeyote: Tundu Lisu
Vifo watu 17: Rais Samia atuma salamu za rambirambi